Swahili version
Mfanyabiashara na Tajiri Namba Moja Tanzania Mo Dewji Amepatikana Maeneo ya Gymkhana Tayari jeshi la police limeweka utepe eneo la tukio lilipotelekezwa Gari lililotumika kumtelekeza Mo, Familia Tayari Imetoa taarifa juu ya kupatikana kwake,Jeshi la police kuongea na Wananchi kupitia vyombo vya Habari. Baada ya Uchunguzi mfupi unaofanyika Gymkhana silaha mbali mbali zimekutwa kwenye Gari Hilo.Ata hivyo kamanda Lazaro Mambo sasa amesema watu waliomteka walikuwa wanataka fedha.Akiongea leo nyumbani kwa baba yake Mo ambako alifika kumuona mfanyabiashara huyo, amesema amemweleza kuwa moja ya sababu ya kutekwa kwake ni fedha ambapo watekaji walikuwa wanataka wapewe fedha.
”Mo ameniambia tangu alipotekwa alikuwa amefungwa mikono, miguu na kufunikwa macho, lakini pia walimsimamia sana kwenye suala la kula lakini sababu kubwa watekaji walikuwa wanataka fedha ila walikuwa na hofu ya kumpigia baba yake wakiamini jeshi la polisi litawafikia”, amesema Mambosasa
Pia Mambo sasa ameongea kuwa baada ya taarifa za jana kutoka kwa IGP Sirro kubaini gari lililotumika kumteka, zimesaidia kumpata mfanyabiashara huyo kwani wahusika waligundua wamekaribia kunaswa.
Kamanda Mambosasa pia amethibitisha kuwa gari lenye namba za usajili T 314 AXX, ambalo walilibaini kutumika kumteka Mo, likiwa na namba za nchi jirani AGX 404 MC, ndio hilo limetumika kumtelekeza katika eneo la Gymkhana jijini Dar es salaam.
Amemaliza kwa kusema baada ya kutupwa pale Gymkhana, walinzi wa eneo hilo walimuona na kumtambua kama ni Mo, ndipo wakamfungua kamba alizokuwa amefungwa kisha akawatajia namba za simu za baba yake na walipompigia mzee Dewji akafika na familia kumchukua Source: http://dar24.com/hii-ndio-sababu-ya-mo-dewji-kutekwa/
No comments:
Post a Comment