Skip to main content

Serikali Yaajiri walimu Wapya 4,549 ,Majina na shule zao Hapa

SWAHILI VERSION
                                                                                               
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ''TAMISEMI''  ameutangazia umma  jumla ya walimu 4,549 waliochaguliwa  wamepangiwa kufundisha katika shule za msingi na Sekondari.

Kwa mujibu wa Waziri Huyo Seleman Jafo ni kwamba TAMISEMI ilipata kibali cha kuajiri jumla ya walimu 4, 549 na kibali hicho kilikuwa kwa ajili ya walimu was shule hizo na hasa katika maeneo yaliyo na upungufu.

Akizungumza leo Aprili 27,2019 jijini Dar es Salaam  Seleman Jafo amesema jumla ya waombaji 91,108 waliotuma maombi ya nafasi mbalimbali zilizotangazwa na kati yao maombi 43,770 sawa na  48.04% ya waombaji wote walikuwa na viambatanitisho  vyote vilivyohitajika. Ameongeza na jumla ya waombaji 47,338 sawa na  51.96% maombi yao hayakuwa na vigezo ikiwa ni pamoja na kukosa viambatisho muhimu vilivyohitajika.

E-money exchanger rating
"Kutokana na mahitaji makubwa ya walimu katika shule za msingi na walimu wa shule za msingi wa masomo ya sayansi(Fizikia,Kemia na Bailojia) na hisabati .Ofisi ya TAMISEMI imefanya uchambuzi na kutoa kipaumbele katika ajira ya walimu wa kada za walimu daraja la tatu A(cheti)kwa ajili ya kufundisha shule za msingi.

Walimu daraja la tatu B (Stashahada)
 wa masomo ya sayansi kwa ajili ya kufundisha shule za sekondari kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.Walimu daraja la tatu C wa masomo ya sayansi kwa ajili ya kufundisha katika shule za sekondari za kidato cha tano na sita.

Na walimu daraja la tatu C (Shahada)  
wa masomo ya elimu maalum ,biashara ,uchumi,kilimo na maarifa ya nyumbani kwa ajili ya kufundisha shule za sekondari. Mchakato wa kupitia maombi ulijumuisha uhakiki wa uhalali wa vyeti vy elimu na taaluma vya waombaji na ukamilifu wa nyaraka zilizohitajika," amesema Jafo.

Amefafanua anatumia nafasi hiyo kuwataarifu waombaji wote wa masomo ya Sana'a ,sayansi na masomo mengine ambao walitimiza vigezo na hawakufanikiwa kupata nafasi katika kipindi hiki kuwa maombi yao yote yamechambuliwa na yamehifadhiwa kwenye kanzidata yao na kuwa fursa za ajira zitakapojitokeza utaratibu wa ajira utatolewa.

Kuhusu walimu waliopata ajira ambao ni hao 4,549 wamepangiwa moja kwa moja na kati ya hao jumla ya walimu 3,059 sawa na asilimia 67.25 wamepangiwa kufundisha shule za msingi na walimu 1,490 sawa na asilimia 32.75 wamepangwa kufundisha shule za sekondari.

"Walimu wote waliopata ajira wanatakiwa kuripoti kwa wakurugenzi wa halmashauri zilipo shule walizopangwa kwa ajili ya uhakiki wa vyeti halisi vya elimu na taaluma,kujaza mikata ya ajira na taratibu nyingine za kiutumishi na kisha kuripoti katika shule walizopangiwa.

" Walimu wote waliopata ajira wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya Nazi kuanzia Mei 7,2019 hadi Mei 21,2019 .Walimu wapya ambao hawataripoti katika vituo vyao vya kazi ifikapo Mei 21,2019 nafasi zao zitajazwa mara moja bila kuwataarifu kwa kuwapanga walimu wenye sifa ambao hawakupangwa katika awamu hii.

"Aidha Wakurugenzi wa halmashauri wasibadilishe vituo vya kazi  vya walimu hao bila kibali maalum cha Katibu Mkuu TAMISEMI .Mwajiriwa atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu kisha akaondoka katika kituo chake cha kazi alichopangiwa atachukuliwa hatua kali za kisheria," amesema Jafo.

Pia amewomba wakurugenzi wote wa halmashauri zilizopangiwa walimu wa ajira mpya kuwapokea walimu hao na kukamilisha taratibu za ajira kwa kuzingatia sheria ,kanuni ,taratibu na miongozo inayosimamia utumishi wa umma  

  WALIMU WALIOCHAGULIWA NA KUPANGIWA SHULE ZA MSINGI

  
 2     WALIMU WALIOCHAGULIWA NAKUPANGIWA SHULE ZA SEKONDARI                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                         

Comments

Popular posts from this blog

FINANCIAL FREEDOM WITH DIGITAL CURRENCIES

FINANCIAL FREEDOM WITH DIGITAL CURRENCIES   Pay attention to the financial systems that try to give freedom in making transactions in everyday life, many businesses have been opened to enable someone or people to earn a daily income. Free markets from local markets to the internet have also increased to empower and empower people to achieve their goals, at the same time companies have been using that opportunity to make profit from daily transactions, this is definitely a revolution of satisfaction for people. All these steps have been attacked by various emotions, the emotions of young people have grown, and I have prioritized them in moving forward these non-Isha raids. Let's see this which is not many years old and has survived and is going to save the youth In recent years, new systems have emerged which were not widely understood in our Communities, few of them have been using those systems, known as digital investment, to invest in DIGITAL CURRENCIES.  DIGITAL CURRENCIES...

UDHIBITI WA CHANGAMOTO ZA MADENI

Kudhibiti madeni yaliyozidi uwezo wako wa kulipa ni jambo linalohitaji mpango mzuri na nidhamu ya kifedha. Hapa kuna hatua unazoweza kuchukua ili kuanza kurekebisha hali yako: 1. Tafuta Chanzo cha Tatizo Je, ni matumizi mabaya ya pesa? Je, ni kupungua kwa kipato? Je, ni dharura ambazo hazikupangwa? Ukigundua chanzo, utaweza kuepuka kurudia kosa hilo. 2. Fanya Tathmini ya Madeni Yako Andika orodha ya madeni yako yote (benki, watu binafsi, mikopo ya biashara n.k.). Weka kipaumbele kulingana na riba kubwa na madeni yanayoweza kuleta athari mbaya haraka (kama kukatwa mali). 3. Wasiliana na Wadai Badala ya kukwepa, zungumza nao kuhusu hali yako halisi. Omba mpango wa malipo wa muda mrefu au punguzo la riba ikiwa linawezekana. 4. Tengeneza Bajeti na Uifate Punguza matumizi yasiyo ya lazima. Elekeza pesa kwenye madeni badala ya matumizi ya anasa. Tumia kanuni ya  50/30/20  (50% mahitaji, 30% starehe, 20% madeni na akiba). 5. Tafuta Njia za Kuongeza Kipato Tafuta kazi za ziada kama fr...

Moussa Balla Conte

Moussa Balla Conte ajiunga na Yanga SC!  ðŸŸ¡⚫️ Leo, Moussa Balla Conte ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa Klabu ya Yanga SC, akitokea CS Sfaxien ya Tunisia, baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu. Hii ni baada ya sintofahamu kubwa kuhusu usajili wake, huku habari zikimhusisha na Simba SC. Lakini, Yanga SC imefanikiwa kumchukua Conte, na sasa huduma zake ni mali ya Wananchi kuelekea msimu mpya. Kwa usajili huu, unawapa Wananchi asilimia ngapi ya mafanikio ya usajili? 👉 Je, Conte ni mchezaji ambaye ataongeza nguvu kwenye safu ya kiungo wa Yanga SC? #YangaSC #MoussaBallaConte #Wananchi #Usajili #Soka #Tanzania #Mchezo