Nairobi, Kenya
Taifa la Kenya limeingia katika kipindi cha majonzi makubwa kufuatia kifo cha kiongozi wa upinzani na mwanasiasa mashuhuri, Raila Amolo Odinga. Tukio hili limeleta athari si tu kisiasa bali pia kiuchumi, huku shughuli nyingi za biashara na huduma zikiwa zimesimama kwa siku kadhaa kote nchini.
Miji mikubwa kama Nairobi, Kisumu, Mombasa, Eldoret na Nakuru imeshuhudia utulivu usio wa kawaida. Wafanyabiashara wengi wamefunga maduka, magari ya usafiri yamesimama, na hata baadhi ya taasisi za serikali zimetoa ruhusa kwa wafanyakazi kuhudhuria shughuli za kumuaga kiongozi huyo.
“Raila Odinga alikuwa ni zaidi ya mwanasiasa alikuwa ni alama ya matumaini. Ni kawaida kuona wananchi wakisimamisha shughuli zao kumheshimu mtu wa aina hiyo.”
Katika maeneo mengi ya nchi, wananchi wameonekana wakifanya maandamano ya amani, wakiimba nyimbo za kumbukumbu na kushika mabango yenye ujumbe wa heshima na upendo. Wengine wamepamba mitaa kwa bendera nusu mlingoti na picha za Raila, wakionesha jinsi alivyogusa maisha ya wengi.
Serikali ya Kenya imetangaza siku kadhaa za maombolezo ya kitaifa, huku viongozi wa mataifa mbalimbali wakitarajiwa kuhudhuria mazishi hayo ya kihistoria.
Kwa sasa, Kenya ipo katika hali ya utulivu wa heshima taifa lote likiwa limetulia kumuaga shujaa wa demokrasia, Raila Amolo Odinga (1945–2025).
No comments:
Post a Comment